Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa...

12
MUKHTASARI Mtazamo wa SymbioCity MFUMO NADHARIA WA USTAWISHAJI ENDELEVU WA MIJI

Transcript of Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa...

Page 1: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 1

MUKHTASARI

Mtazamo waSymbioCity

MFUMO NADHARIA WA USTAWISHAJI ENDELEVU

WA MIJI

Page 2: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

2 | Mtazamo wa SymbioCity | MUKHTASARI – 2012

MAELEZO YA UHARIRIwaandishi Prof. Ulf Ranhagen, Royal Institute of Technology (KTH) Klas Groth, Urban Advisor, SKL Internationalusanifishaji bunifu na michoro Viera Larsson, Ordbildarna AB na waandishiuhariri wa kiingereza John Roux, Ordbildarna ABusaidizi wa uhariri Paul Dixelius na Lena Nilsson, SKL International

© Hakimiliki – SKL International, 2012

anwani

SKL International, Stockholm, Swedentovuti www.sklinternational.se barua pepe [email protected] simu +46 8 452 70 00

Page 3: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 3

»Jiji si tatizo– ni suluhu«

Jamie Lerner aliyekuwa Meya wa Curitiba,

Kuchipuka na kuenea kwa miji kunatokea hasa katika mataifa yanayoen-delea, na ongezeko la idadi ya watu siku za usoni huenda likashuhudiwa

katika majiji na miji pekee katika mataifa ambayo hayajaendelea. Kila mwaka, takriban watu 50 milioni (au 140 000 kila siku) huhamia mijini, na hasa katika mitaa ya mabanda.

Ni vigumu sana kwa miji kukosa kuendelea kuchipuka na kuenea kwa kuwa miji hutoa nafasi bora za elimu, masuala ya kijamii na kiuchumi na pia huduma bora, na huwa pia vitovu vya ukuaji wa kisiasa, kitamaduni na kiu-chumi. Hata hivyo, ukuaji wa haraka wa mitaa duni unatoa changamoto kub-wa, ambazo zinahitaji mikakati oanishi ya kiufundi, kifedha, kijamii na katika upangaji wa miji na maendeleo ili kuhakikisha kuna mazingira bora na endel-evu mijini na pia hali nzuri ya maisha.

Kuwepo kwa watu wengi mijini hutoa fursa bora kwa ustawishaji wa hu-duma muhimu kama vile uchukuzi, utumiaji tena wa maji, taka na vitu ving-ine, pamoja na utumiaji bora wa kawi. Hata hivyo, matatizo ya ueneaji wa miji hutawala mjadala kuhusu miji, na ni nadara kwa manufaa kupatikana katika miji ya mataifa yanayoendelea. Kama vitovu vya kiuchumi na wachangiaji muhimu wa Mapato Ghafi ya Ndani (GDP) miji, inafaa kuwa na uwezo na ra-silimali za kifedha kukabiliana na changamoto za ueneaji wa miji, hasa kwa makundi ya wasiojiweza.

Miji ina athari kubwa kimazingira kutokana na ‘uzito’ wa kuishi watu wengi na kiasi cha maliasili wanayotumia. Kila sehemu ya maisha mijini huwa na athari kwa dunia, na hasa kawi inayotumiwa na mabilioni ya watu na magari barabarani, kutia joto au kupoza hewa katika majumba, na kutoa chakula na rasilimali nyingine, hasa kutoka pande nyingine za ulimwengu. Kawi kutoka kwa visukuku na kuwepo kwa magari yasiyotumia vyema kawi huchangia sana utoaji wa gesi ya co2 inayozidisha ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa.

Maskini ndio wanaoathiriwa zaidi uharibifu wa mazingira kutokana na uchafuzi wa maji na hewa, kemikali zenye sumu, mafuriko, tsunami, ukame na maporomoko ya ardhi. Wakazi maskini wa mitaa duni sana huwa pia hawana haki za umiliki wa ardhi na hawawakilishwi katika mipango ya ustawishaji wa miji na ugawaji wa rasilimali.

Haki zao za kibinadamu za uhai, afya, maji safi ya kutosha, chakula, makazi na huduma za serikali huhujumiwa kwenye mazingira yaliyochafuliwa.

Tangu mwanzo wa karne hii, sehemu kubwa ya watu duniani wameishi mijini. Inakadiriwa kwamba idadi ya watu duniani itaongezeka kutoka 7 bilio-

Tangu mwanzo wa karne hii, sehemu kubwa ya watu duni-ani wameishi mijini. Inakadi-riwa kwamba idadi ya watu duniani itaongezeka kutoka 7 bilioni hadi 9 bilioni kufikia 2050, na kwamba 60% ya watu wataishi mijini kufikia 2030, na 70% kufikia 2050.

Kubadilisha changamoto katika miji kuwa manufaa

pich

a U

lf R

anha

gen

pich

a B

uffa

lo C

ity M

unic

ipal

ity, S

outh

Afr

ica

Page 4: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

4 | Mtazamo wa SymbioCity | MUKHTASARI – 2012

ni hadi 9 bilioni kufikia 2050, na kwamba 60% ya watu wataishi mijini kufikia 2030, na 70% kufikia 2050.

Changamoto za kimazingira hutokana sana na shughuli za kiuchumi, ambazo zina msingi wake katika maadili ya kitamaduni, mitazamo na tabia katika jamii inayoangazia zaidi matumizi. Maskini hutamani kuishi maisha ya kifahari ya mataifa tajiri, lakini hii itahitaji kutumia rasilimali kwa kiwango cha juu kisichowezekana. Mtindo huu wa maisha wa kutumia vitu kwa wingi hauwezekani kwa wote na hauwezi kuendelea kwa muda mrefu, hata katika mataifa tajiri. Kwa hivyo, kubadili mtazamo wetu ili kuwezesha miji endelevu siku za usoni kunahitajika.

Kwa Mtazamo wa SymbioCity, usawa katika kupokea huduma za kimsingi za miundo msingi na kijamii umepewa umuhimu mkubwa. Hili linaweza ku-fanikishwa kukiwa na maeneo yenye watu wengi, ya matumizi mseto yenye mchanganyiko wa huduma za kibinafsi na umma, nafasi nzuri za kazi na ku-zalisha mapato, na kuimarishwa kwa maeneo ya umma. Utawala bora wa miji na upangaji stadi ni muhimu sana katika kuimarisha hali ya maisha ya makun-di ya watu maskini na wasiojiweza. Kuimarishwa kwa nafasi za kupata elimu, huduma za afya na nafasi za kiuchumi ni muhimu kwa ustawi wa usawa wa kijamii na kiuchumi.

Usalama pia ni muhimu, na mipangilio mahsusi ya miji inaweza kupele-kea kuwepo kwa mitaa, maeneo ya umma na miundo msingi inayofanikisha ufuatilizi, uchunguzi, usalama na uhusiano bora wa kijamii. Kupatikana kwa maeneo yenye miti na nyasi na maeneo ya michezo na burudani ni muhimu sana, sawa na shule, makanisa, maktaba na kadhalika. Mazingira yaliyopang-wa na kujengwa vyema husisimua uhusiano bora katika jamii na umiliki wa maeneo ya umma, jambo ambalo husaidia ukuaji wa jamii.

Masuala ya kijamii na kitamaduni na hali ya maisha moja kwa moja huathiri ukuaji wa miji kiuchumi na kimazingira. Lengo kuu la ustawishaji wa miji endelevu linafaa kuwa kufanikisha mazingira bora katika miji, ambayo ni thabiti na endelevu, kwa jamii zote. Nguvu zote zinafaa kuelekezwa katika ku-punguza umaskini na kuimarisha mapato ya familia, viwango vya maisha, hali njema ya watu kwa jumla na usalama.

Maeneo ya miji ni ‘injini’ za kufanikisha ustawi wa kitamaduni, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Ingawa upangaji wa miji unafaa kusaidia miradi na shu-ghuli za kiuchumi, hili linafaa kusawazishwa na mahitaji ya kijamii, kitama-duni na kimazingira na mzigo kwa rasilimali. Ukuaji endelevu wa uchumi un-aweza kufanikishwa kupitia uimarishaji wa usimamizi wa maeneo, ustawi wa matumizi mchanganyiko ambao unasaidia ujasiriamali, na ushirikiano kati ya sekta za kibinafsi, wasomi na serikali.

Jiji endelevu au eco-city limejengwa kupunguza athari mbaya za kimazingira.

pich

a Vi

era

Lars

son

pich

a M

ats

Ögr

en W

ange

r

Page 5: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 5

Kakati huu wa kidhana ni wa jumla na unaweza kutumiwa kwa urahisi ka-tika maeneo yoyote ya miji. Unatoa mwongozo wa jumla na njia za ku-

saidia kufanikisha ustawishaji endelevu wa miji. Malengo ya Mtazamo wa SymbioCity ni

> Kufanikisha na kusaidia ushirikiano wa fani nyingi kati ya washikadau na kwa mtazamo unaohusisha wote

> Kuchangia katika kuimarisha uwezo kwa kugawana habari na ujuzi, hasa katika ngazi ya serikali za mitaa

> Kutumika kama msingi wa kuanzisha mashauriano na ushirikiano kati ya washikadau ngazi ya mashinani, lakini pia ngazi ya jimbo na taasisi za kitaifa

> Kuongoza utathmini wa uendelevu wa miji katika ngazi tofauti kwa ku-tumia mtazamo wa kushirikisha fani na sekta nyingi

> Kuchangia mikakati ya kushirikisha maeneo yote ya miji katika kuimarisha maeneo ya miji, ikihusisha fani zote za uendelevu

> Kusaidia majiji na miji kupanga mifumo husishi na inayoweza kutekeleze-ka ya kuhakikisha ustawishaji endelevu wa miji

Ustawishaji endelevu wa miji ni fani changamano, ambayo huhusisha mi-fumo mingi, huduma na uhusiano. Mtazamo wa SymbioCity unatoa taswira ya juu ya masuala mengi, vihusishi, nyuso na nguvu zinazohusika kati ya mi-fumo, fani na majukumu ambayo yanafaa kuzingatiwa katika mradi wowote wa ustawishaji wa mji.

Mkakati huu wa kidhana unatilia mkazo shughuli bora za maendeleo na taratibu bora za kufanya kazi, ambazo zinaweza kujumuisha utathmini wa umaskini na mapendekezo ya kukabiliana na umaskini. Hata hivyo, mkakati huu haujatathmini kwa kina fani za kitamaduni na kijamii au kiuchumi za ustawi. Umeangazia zaidi fani za mazingira, nafasi na mifumo kuhusiana na uendelevu katika miji, lakini pia kwa kuzingatia uhusiano na fani nyingine.

Mtazamo wa SymbioCity unafaa kusaidia badala ya kuchukua nafasi ya mikakati iliyopo ya kisheria pamoja na sera. Madhumuni yake ni kutoa usaidi-zi wa njia, vifaa na taratibu kwa miradi ya ustawishaji endelevu wa miji, na ku-fungamanisha na kufafanua mahitaji mbalimbali, mitazamo, na makusudio. Jinsi mtazamo huu utatumiwa, inafaa kutegemea eneo lenyewe na upatikanaji wa rasilimali za kiuchumi, kiufundi na watu.

Mtazamo huu pia unatambua mitazamo mingine mingi kuhusu ukuaji wa miji, na kusudi lake ni kushirikiana badala ya kushindana na mitazamo mingine ambayo ina maslahi sawa na malengo sawa.

Udadisi wowote wa ustawishaji wa miji au mahitaji ya miradi unafaa kuzingatia hali ya watu maskini na wasio na uwezo, ambao hukosa kuwakil-ishwa, na huwa hawahusishwi kwenye mipango na utoaji wa maamuzi yanay-owaathiri. Mwongozo huu hauwezi kuangazia hili kwa kina kwa sasa, lakini masuala ya kiutawala na ushirikishi katika ustawishaji wa miji yamejadiliwa katika sura kuhusu mambo ya kitaasisi.

Mtazamo wa SymbioCity huhimiza njia husishi na ya kuzingatia fani nyingi kuan-gazia ustawishaji wa miji, ambayo inafaa mataifa ya-nayoendelea, yaliyo kwenye mpito, na yaliyoendelea.

MTAA MDOGO

MTAA MDOGO

KATIKATI MWA JIJI

WILAYA WA MJI

ENEO LA MASHAMBANI

ENEO LA MASHAMBANI

Mtazamo wa SymbioCity – madhumuni na upana wake

Mtazamo wa SymbioCity unaweza kutumiwa kama mpangilio wa kidhana na kuongoza shughuli za ustawishaji endelevu wa miji.

Mtazamo wa SymbioCity – MFUMO NADHARIA

MIFUMO YA MIJI

MAMBO YA KITAASISI

MPANGILIO NADHARIA

CHAN

GAM

OTO

MIJINI

TARATIBU ZA KUFANYA KAZI

MIFANO

Mtazamo wa SymbioCity husisitiza ustawi wa miji kuambatana na eneo husika, na hivyo uhusiano kati ya miji, vituo vidogo vya miji na maeneo ya mashambani.

Page 6: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

6 | Mtazamo wa SymbioCity | MUKHTASARI – 2012

Mtazamo wa SymbioCity unatoa mkakati wa kidhana na mwongozo rahisi na njia za kufanikisha upangaji wa

ustawishaji endelevu wa miji.

Mtazamo wa SymbioCity kama njia

Kanuni ya mtazamo wa fani nyingi (juu)Na mtazamo wa kisekta (chini).

Mtazamo wa SymbioCity ni muhimu kwa > Kuanzisha na kuelekeza shughuli za kupanga ustawishaji > Kufanya utathmini wa uendelevu katika ngazi mbalimbali > Kufafanua mikakati ya ustawishaji kwa miji iliyopo au maeneo mapya ya

miji au majiji > Kudadisi mikakati ya kitaasisi na kiutawala.

Mtazamo huu unajumuisha vihusishi na uhusiano kati ya ustawi wa miji na maeneo ya mashambani, pamoja na miktadha ya kitaifa na kimataifa.

Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo ya Miji. Kila jambo linaweza kuangaliwa kivyake, kulingana na muktadha, malengo na mtazamo wa shughuli yenyewe. Hata hivyo, ni muhimu kawaida kuunganisha mambo haya matatu, jambo linaloweza kufanyika kwa njia tatu tofauti.

Kwa mfano, unapopanga kuhusu mfumo fulani kama vile wa maji, taka au kawi, mambo ya kitaasisi kama vile utawala kawaida ndiyo huamua ufanisi wa mradi. Mpangilio wa Kidhana unaweza kutumiwa kuamua uendelevu ka-tika muktadha wa eneo mwenyeji, kutambua uhusiano unaowezekana kati ya mifumo ya miji, na kuunganisha fani za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Mtazamo wa SymbioCity unasisitiza mtazamo wa fani nyingi, lakini un-aweza kutazamwa kwa njia mbili kuu.

1. Mtazamo wa fani nyingi ambao unatathmini eneo fulani kutoka njia mbal-imbali, kutambua uhusiano baina ya mifumo mbalimbali katika mkakati husishi wa mipango. Hii inahitaji shughuli huru na wazi kuanzia mwanzo, kukabiliana na vikwazo vya kitaasisi vinavyoweza kuchipuka au mgongano wa maslahi.

2. Mtazamo wa kisekta unaoangazia mfumo fulani wa mji, kwa mfano maji, lakini kisha unapanua upana wake na kutambua uhusiano unaowezeka-na kati yake na mifumo mingine yenye uhusiano wa karibu. Mtazamo wa kisekta unaweza kukua baada ya muda na kuwa mtazamo wa fani nyingi.

pich

a U

lf R

anha

gen

Page 7: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 7

Hata hivyo, kwa sababu kila jiji au mji una sifa zake, muktadha na changa-moto za ustawishaji, mpangilio huu unafaa kufanyiwa mabadiliko uwiane

na hali katika eneo husika na kwa madhumuni husika.Mpangilio huo unaweza kutumiwa kusaidia utathmini wa uendelevu wa

miji na mpango ya ustawishaji wa miji katika ngazi mbalimbali, na kutafuta suluhu. Mpangilio wa kidhana unasisitiza uhusiano uliopo kati ya fani za maz-ingira, kijamii na kitamaduni, na maeneo katika uendelevu wa miji. Pia unatoa mkakati wa kueleza uhusiano kati ya majukumu mbalimbali na mifumo katika miji, ili kutambua na kukuza uhusiano kati ya mifumo hiyo.

Lengo kuu la ustawishaji ambalo ni maisha bora, ikiwemo afya na usala-ma kwa wote, limo katika kitovu cha mpangilio huu.

Mviringo wa kwanza unawakilisha fani za kimazingira, kiuchumi na ki-jamii na kiutamaduni na changamoto katika uendelevu wa miji. Mviringo wa pili unawakilisha mifumo ya miji ya maji, kawi, uchukuzi na trafiki, uzoaji taka, mawasiliano na maeneo yenye nyasi na miti pamoja na maeneo mengine ya umma. Majukumu yote ya miji na vitu tunavyotumia kila siku vimeelezwa kama mifumo ya miji (kwa mfano, makazi, maeneo ya kazi, maeneo ya kijamii na majengo ya biashara, na kadhalika).

Mviringo wa tatu unawakilisha mifumo ya kitaasisi na utawala ambayo husaidia na kuathiri majukumu ya miji na ustawishaji endelevu. Fani ya nne ya mpangilio huu inawakilisha mazingira ya kujengwa na ya kiasili, na muktadha wa nafasi za hatua zozote za kufanikisha uendelevu wa mij

Mpangilio wa kidhana kwa uendelevu wa mijiUS

IMAM

IZI W

A AR

DH

I •

UPA

NGA

JI W

A MIJI

• U

TAWALA WA MIJI • SHERIA & SERA • TEKNOLOJIA • KUSHIRIKISHW

A KW

A UM

MA •

• FEDHA • MAFUNZO NA ELIMU • USHIRIKIANO WA UMMA NA SEKTA YA

KIB

INAF

SI

TOPO

GRAPHY

U

UNGANISHI WA MAENEO UNGANISHI WA M

IJI/MAEN

EO YA M

ASHAM

BANI

UK

UBWA UPANGAJI WINGI WA WATU

• TRAFIKI/U

CHUK

UZI

• ICT

• MAJ

UM

BA / M

AJUMBA/U

SANIFU MIJENGO • MAJUKUMU YA MIJI & MIFUM

O • MAN

DH

ARI/M

AENEO YA UMMA •

TAKA • MAJI • KAWI

MABADILIKO YA HALI YA HEWA •HATARI

UCHAFUZI • SUMU MIALI NURURISHI

HAKI •KUSHIRIKISHWA KW

A JAMII

MAENDELEO YA W

ATU

KUVUMILIANA • IDADI YA W

ATU

MILA &TAM

ADUNI UVU

MBU

ZI •

UTA

JIRI

WA

MIJ

I

CMAT

UMIZ

I & U

ZALI

SHAJ

I

UKUA

JI W

A KI

UCHU

MI

Mpangilio wa kidhana kwa mtazamo husishi na timilifu wa ustawishaji wa miji. Mpangilio huu unaonyesha fani za kimazingira, kijamii na kitamaduni, kiu-chumi, nafasi, kitaasisi na mifumo katika ustawishaji endelevu wa miji, na mifano ya mambo muhimu katika kila fani kuu iliyotajwa.

Mtazamo wa SymbioCity unafanikisha utathmini wa shughuli za utathmini na mipango katika miji ambazo zinazinga-tia uhusiano kati ya mifumo na ambao unaweza kuongeza thamani katika fani za kimazingira, kiuchumi, kijamii na kitama-duni na kinafasi katika ustawishaji.

Mpangilio wa kidhana wa mtazamo wa Symbio City Approach ni wa kijumla na unajumuisha masuala mengi ya ustawishaji wa miji na uhu-siano unaofaa kuangaziwa.

MAJUMBA

MAN

DHARI/MIFUM

O YA VIUMBE HAI

M A JITAK A

MAENEO YA UMM

AKIJA

MII N

A KITAMADUNI

K

IUCH

UMI

MAMBO YA

KIMAZINGIRA

MAM

BO YA

MAMBO

YA

ICT

TRAFIKI/UCHUK

UZI

KAWI

MAJUKUMU YA MIJI

Page 8: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

8 | Mtazamo wa SymbioCity | MUKHTASARI – 2012

Mtazamo wa SymbioCity, unajumuisha mambo makuu yafuatayo.

Utawala wa miji na uwezeshajiUtawala bora wa miji ni muhimu sana kwani hujumuisha usimamizi wa rasili-mali za kifedha, kiuchumi, kiufundi, kishirika, wafanyakazi na rasilimali ny-ingine zinazohitajika kuimarisha mazingira ya miji. Benki ya Dunia imeeleza utawala bora kuwa » Utayarishaji sera wazi, wa kutabirika na unaoongozwa na maarifa, watawala wanaoongozwa na maadili ya kitaalamu wakifanya kazi kwa maslahi ya umma, utawala wa sheria, mifumo wazi, na mashirika thabiti ya kijamii yanayoshiriki masuala ya umma.«

Sheria na seraSheria na sera kuhusu mazingira katika miji ni njia muhimu za kuhakikisha uboreshaji, kwa jumla na kwa maskini wanaoishi mijini. Sheria za Kitaifa na kieneo na malengo ya kisera kuhusu mazingira mijini zinafaa kuwa kidato cha kwanza katika kupanga sera za eneo husika, kanuni za mipango na sheria za ujenzi wa nyumba.

Mpangilio wa nafasi zilizopo na usimamizi wa ardhiUpangaji kuhusu nafasi unahusisha kuratibiwa kwa aina zote za vipande vya ardhi katika miji na maeneo ya mashambani. Muingiliano kati ya maeneo ya miji na mashambani ni muhimu sana kwa ustawishaji endelevu. Shughuli za kupanga miji zinafaa kuhusisha washikadau wote na kusawazisha maslahi mbalimbali katika mashauriano ya umma, ushirikishi, na ufanyaji maamuzi ulio wazi. Mifumo ya usimamizi wa ardhi inafaa kulainishwa iambatane na malengo ya upangaji wa miji. Sheria na sera zinazoweza kuimarisha hali ya maisha kwa maskini kwa kuhimiza ploti ndogo, matumizi mseto ya ardhi na kutokuwa ghali sana kwa ardhi na miundo msingi ya utoaji makao.

Shughuli za kushirikisha ummaKushirikishwa kwa umma katika juhudi za kuimarisha mazingira ni muhimu kwa madhumuni ya ufanisi kipindi kifupi na kirefu. Ni muhimu kufahamisha wakazi kuanzia mwanzo na kuwepo mikakati ya kushirikisha umma na kuz-ingatia mchango wao katika shughuli za kutathmini, kupanga na kutekeleza na pia kufuatilia. Haiwezekani kuhusisha kila mtu, lakini taasisii wakilishi na makundi ya kijamii yanafaa kuombwa ushauri na kushirikishwa.

Rasilimali za kifedha na vichocheoUfadhili mwema ni muhimu katika kupanga na kutekeleza hatua za kuima-risha mazingira ya miji. Utaalamu wa kifedha unahitajika kuanzia mwanzo kutoa taswira pana ya mahitaji ya kifedha na hatari zilizopo, na kutoa mpango halisia wa fedha zinazohitajika.

Kushirikishwa kwa sekta ya kibinafsiUshirikiano unaoendelea kati ya wasimamizi wa miji na sekta ya kibinafsi ni muhimu sana katika kupanga majiji na miji endelevu. Kunafaa kuwa na vi-chocheo kwa biashara za viwango mbalimbali kujishirikisha katika ubadilishaji wa miji. Fani mbalimbali za utoaji ushauri na utengenezaji bidhaa zinaweza kutoa ushauri na mifumo na bidhaa bunifu na endelevu.

Mambo ya kitaasisi

pich

a Pe

ter

Engs

tröm

pich

a U

lf R

anha

gen

Mkakati mwema wa kitaasisi unahitajika kufanikisha

ustawishaji endelevu wa miji na kuboresha mazingira ya

miji.

Page 9: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 9

Maeneo ya miji hujumuisha majukumu, mifumo na huduma ambavyo vimesambazwa katika maeneo mbalimbali na vina uhusiano, moja kwa

moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Ili kufanikisha uendelevu na kuanga-zia changamoto za kimazingira, kijamii na kitamaduni, na kiuchumi, Mtazamo wa SymbioCity huangazia uhusiano kati ya mifumo ya miji, ikiwa ni pamoja na mifumo ya kiufundi, kiviumbe na kielimu na kijamii na kitamaduni na pia kiuchumi.

Mifumo ya miji na miundo msingi inayotoa huduma za kimsingi ni maji, taka na kawi, mazingira yenye nyasi na miti mijini na mifumo ya viumbe hai, uchukuzi, mijengo, na kadhalika. Majukumu ya miji yana uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya kila siku na yana uhusiano pia na huathiri fani za kimazingira, kiuchumi na kijamii na kitamaduni za ustawi wa miji. Majukumu ya miji ni pamoja na makazi na ujenzi wa nyumba za makazi, uzalishaji wa kiviwanda, shughuli za kibiashara, utamaduni na burudani, elimu, afya na hu-duma za kijamii.

Mifumo hii yote ya miji ni muhimu kwa ustawishaji endelevu wa miji. Huhusiana kwa njia tofauti na fani nne za uendelevu, jambo ambalo lina-dokeza umuhimu wa mtazamo changamano na wa kuhusisha sekta zote katika ustawishaji.

Majukumu ya miji, huduma, na mifumo ya miundo msingi yanafaa kupa-tikana kwa wote na kwa bei nafuu, na kwa kuwa ustawishaji wa miji huhitaji uwekezaji, mifumo ya kutosha ya utoaji pesa ni muhimu. Utawala bora na uw-ezo wa kitaasisi pia ni muhimu, na mahitaji ya raia, na hasa maskini na watu wasiojiweza yanafaa kupewa kipaumbele.

Mtazamo wa SymbioCity unaangazia uhusiano uliopo baina ya mifumo hii kuzuia kutotumiwa vyema kwa uwezo wote na kupata suluhu bora zaidi na matumizi bora ya rasilimali. Hata hivyo, uhusiano huu unaweza tu kutambuli-wa na kufikiwa kwa kuhusisha washikadau wote katika mtazamo changamano wa ustawishaji, ambao unahusisha fani za kiuchumi, kimazingira, kijamii na kitamaduni na mahitaji.

Mifumo endelevu ya miji na uhusiano

pich

a N

elso

n M

ande

la B

ay M

unic

ipal

ity, S

outh

Afr

ica

Mtazamo wa SymbioCity huangazia uhusiano kati ya mifumo ya miji, pamoja na mambo ya kitaasisi, katika muktadha wa nafasi.

MFANOUhusiano kati ya uchukuzi na mpangilio wa matumizi ya ardhi Upangaji husishi wa matumizi ya ardhi kwa majukumu mbalimbali ya miji unafaa ku-ratibishwa na mfumo husishi wa uchukuzi Hili linaweza kupunguza hitaji la uchukuzi, na kupunguza mahitaji ya matumizi ya kawi na hivyo utoaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani. Wingi wa watu na mpangilio bora wa majukumu mbalimbali ya miji huathiri sana urahisi wa kusafiri. Kuwepo kwa watu wengi katika vitovu vya uchukuzi na karibu na barabara kuu ni njia bora ya kueneza matumizi ya uchukuzi wa umma na kupunguza msongamano mijini.

FEDHA

M A M B O YA N A FA S I

MAM B O YA K I TA A S I S I

M I F U M O Y A M I J I

UCHAFUZI HEWAHATARI

KUTOKA VITU

MBALIMBALI

UCHAFUZI KELELE

AFYAHALI NJE-

MA USALAMAUBORA WA

MAISHA

MAMBO YA KIMAZIN

GIRA

UPANGAJI WA MIJI

TRAFIKI/UCHUKUZI

MAJUKUMU YA MIJI

URBANGOVERNANCE

Page 10: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

10 | Mtazamo wa SymbioCity | MUKHTASARI – 2012

Mtazamo wa SymbioCity unajumuisha shughuli ya jumla ambayo ina-faa kufanyiwa mabadiliko kuambatana na mradi husika na eneo husi-

ka. Shughuli hii ina hatua sita zenye njia mbalimbali na vifaa vya kutumiwa kutekeleza mpangilio wa kidhana wa SymbioCity kwa njia ya mzunguko. Shu-ghuli hii inaweza kutekelezwa katika miktadha mbalimbali ya upangaji, kwa mfano kufanya utathmini wa uendelevu, ustawishaji upya wa maeneo yaliyopo, au kupanga maeneo mapya kwa mizani tofauti ya miji. Ndoto kuu ya kisiasa na malengo inafaa kuwa hatua ya kwanza kwa mtazamo changamano na wa kuhusisha fani nyingi katika kupanga ustawishaji wa miji.

Hatua 1. Eleza na kuandaa shughuli ya kupanga au kutathminiNi muhimu kupanga na kuratibu vyema shughuli ya kutayarisha mpango ndi-po ifanikiwe. Mpango wa kuratibu mambo na pia ratiba vinafaa kuongoza shu-ghuli zote za upangaji na uhusiano. Mpango huu wa kuratibu unafaa kutam-bua na kuhusisha washikadau wote muhimu, kwani ni muhimu kushirikisha raia, na hasa maskini na makundi yaliyotengwa, katika shughuli ya kupanga ustawishaji.

Hatua 2. Tathmini hali ya sasaChangamoto na matatizo katika eneo hilo yanafaa kutambuliwa ili kujua hali, mahitaji, matatizo, nafasi na sifa. Hali ya watu maskini zaidi na makundi ya-siojiweza zaidi inafaa kuangaziwa sana, kwani ndio wanaoathiriwa zaidi na matatizo ya kimazingira katika miji. Ni muhimu sana pia kutambua mali na mambo mema, kwa mfano, kuhusiana na masuala ya kijamii na kitamaduni miongoni mwa mengine.

Viini vya matatizo vinafaa kutambuliwa, kama msingi wa kutayarisha su-luhu bora zaidi na changamano. Unapofanya utathmini wa hali, njia zifuatazo zinaweza kutumiwa:1. Kuchora ramani na michoro ya eneo hilo2. Kuandikwa kwa mambo mema na mabaya3. Utathmini wa mwinamo na mwinuko wa mji 4. Utathmini wa kina wa hali ya mazingira5. Utathmini wa viini na madhara ya matatizo na mambo mema.

Hatua 3. Fafanua madhumuni, viashiria na makusudioMalengo makuu, viashiria na makusudio sasa huandaliwa kwa ajili ya ku-chukua hatua, ambayo itaeleza hali ya usoni ya eneo linaloangaziwa kipindi kifupi, kipindi cha wastani na kwa kipindi kirefu. Malengo haya yanafaa kuon-gozwa na utathmini wa awali na ufafanuzi wa uendelevu wa miji.

Malengo yanaweza kuwa ya ukubwa na viwango vya ubora, na yame-fafanuliwa zaidi kushinda madhumuni. Zifuatazo ndizo hatua za jumla zina-zopendekezwa:1. Fafanua uendelevu wa miji katika eneo husika2. Tambua masuala muhimu ya kuzingatiwa katika upangaji na utathmini3. Tayarisha malengo makuu4. Tayarisha viashiria na makusudio

Utaratibu wa kufanya kazi

Mtazamo wa Kinadharia wa SymbioCity huendeleza utaratibu wazi wa kufanyakazi unaohusisha wote.

pich

a An

na B

ackm

ann

Utaratibu wa kufanya kazi wa Mtazamo wa SymbioCity una-

jumuisha hatua sita zinazo-husiana na njia mbalimbali na vifaa katika njia ya mzunguko.

Page 11: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity| MUKHTASARI – 2012 | 11

Hatua 4. Tayarisha mapendekezo mbadalaNjia mbadala sasa hutambuliwa, kwani changamoto za miji ni ngumu, na sasa huwa kuna suluhu mbadala. Kwa suluhu yoyote au uwekezaji kufaa kwa kip-indi kifupi au kirefu, ni muhimu kwamba njia hiyo mbadala iwe rahisi kureke-bishwa na iangazie uhusiano kati ya mifumo mbalimbali ya miji.

Suluhu zinafaa kuzuia matatizo ya kimazingira, au angalau kuzipunguza. Kurudi nyuma ni njia bora ya upangaji inayotumiwa katika maeneo ya miji yaliyopo na pia maeneo mapya, ambayo huanza kwa kutayarisha maono ya hali inavyohitajika kuwa baadaye, na kisha kutafuta njia za kufikia hali hiyo.

Hatua 5. Kudadisi athariAthari za kiuchumi, kijamii, kimazingira na kinafasi za mapendekezo mbadala au suluhu mseto zinafaa kuchunguzwa na kutumiwa kama msingi wa kufanya uamuzi. Kudadisi athari ni hatua muhimu katika kutayarisha mapendekezo changamano na bunifu, na pia nguzo muhimu ya kufanya utathmini wa uen-delevu.

Utathmini wa Athari za Kimazingira (eias) ni njia iliyotambuliwa sana ya kudadisi athari za kimazingira na faida ya miradi inayopendekezwa, na eias zinaweza kujumuisha athari za kijamii, kitamaduni na kiuchumi.

Hatua 6. Kutayarisha mkakati wa utekelezaji na ufuatiliziPendekezo kamili la mwisho lazima lijumuishe mpango wa utekelezaji na ufuatilizi.

Pendekezo hilo linaweza kuwasilisha njia mbadala inayopendelewa, au kuunganisha njia kadha mbadala. Uhusiano kati ya mifumo mbalimbali ni muhimu pia kuongeza uzuri wa matokeo ya mwisho ya shughuli ya upanga-ji kwa mujibu wa ubora wa mijengo na maeneo yaliyojengwa. Mambo kama vile nafasi na mipango ya uchukuzi, michoro ya nyumba, utoaji wa huduma, maeneo ya umma, upangaji wa mandhari, na kadhalika, yanafaa kufungaman-ishwa katika awamu zote za shughuli ya upangaji na utekelezaji kuhakikisha uendelevu wa kijamii na kitamaduni, kiuchumi na kimazingira.

MZUNGUKO 3

6

5

1

2

34

MZUNGUKO 1

6

5

1

2

34

MZUNGUKO 2

34

6

5

1

2

34

MZUNGUKO 1 MZUNGUKO 2 MZUNGUKO 3

UANDALIZI WA TARATIBU NA UDADISI WA MAPEMA N.K.

MASUALA MUHIMU, MALEN-GO NA NJIA MBADALA N.K.

UTATHMINI WA ATHARI NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI N.K.

Mzunguko wa utaratibu wa kufanya kazi na uhusiano wake na mpangilio wa kidhana.

KUTUMIWA KWA MPANGILIO – SHUGHULI YA KUPANGA/UTARATIBU WA KUFANYA

MAMBO YA NAFASI

MAMBO YA KITAASISI

MIF

UMO YA MIJI

MAM

BO

YA KIJAMII &

MAM

BO Y

A

KITA

MA

DUNI

KIU

CHU

MI

AFYA

STAREHE USALAMA

UHAIUBORA

MAMBO YA

KIMAZINGIRA

hatua 1 +2uandalizi wa taratibu & udadisi wa mapema

hatua 5 +6 utathmini wa athari & mikakati ya utekelezaji

hatua 3 +4 masuala muhimu, malengo & njia mbadala

Page 12: Mtazamo wa SymbioCity - SymbioCity : SymbioCity · Mtazamo wa SymbioCity umeundwa juu ya msingi wa mambo matatu yenye uhusiano – Mpangilio wa Kidhana, Mambo ya Kitaasisi na Mifumo

Mtazamo wa SymbioCity (Mukhtasari) umeandikwa naUlf Ranhagen (mwandishi mkuu) na Klas Groth (mwandishi mwenza), kwa ushirikiano na Paul Dixelius na Lena Nilsson kwa niaba ya SKL International na SALAR (Chama cha Serikali za Mitaa na Majimbo nchini Sweden).

Mchango umetoka kwa wataalamu wengi katika fani ya maendeleo endelevu katika miji kupitia warsha na semina. Wataalamu kutoka UN-Habitat, Mistra Urban Futures, Wizara ya Mazingira ya Sweden, Swedish Trade Council, u-PLAN Tor Eriksson AB na Ulricehamns Kommun, wametoa mchango muhimu kwa kutoa maoni ya kufaa sana na kuchangia sehemu mbalimbali za kijitabu hiki.

Toleo hili la Mtazamo wa SymbioCity limetolewa kutoka kwa »The Sustainable City Approach – Mwongozo wa Sida wa Kusaidia Maendeleo Endelevu ya Miji Kimazingira katika Mataifa Yanayoendelea« (2007), uliochapishwa na Sida INEC/ Urban, pamoja na matoleo ya awali ya Mtazamo wa SymbioCity. Toleo la 2010 pia limetasfiriwa kwa Kichina.